Tovuti hii inaunga mkono watumiaji na waendeshaji wa Mtandao wa Afya Tanzania

 
Kwa kujiunga na Mtandao wa Afya, watoa huduma za afya wenye kadi za simu za Vodacom wanaweza kutumia simu za mkononi kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS) na kupiga simu bure. Wahudumu wa afya wanaweza kutumia huduma hii ya bure kwa mawasiliano ya kitabibu, rufaa za wagonjwa, kuendeleza mafunzo yao kupitia tovuti zilizochaguliwa na zaidi.
 
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pia inatumia mtandao huu kutuma taarifa muhimu kwa wahudumu wa afya kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi (SMS). Taarifa hizi pia zitawekwa kwenye ukurasa wetu wa Facebook, ili kuwapa watoa huduma za afya fursa ya kutoa maoni na kuuliza maswali.
 
Mpango huu unafanyika kwa ushirikiano wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Vodacom, Chama cha madaktari Tanzania, mabaraza ya kitaaluma ya watoa huduma za afya pamoja na IntraHealth International.